Home Uncategorized SABABU KUBWA ZA KAHATA KUMALIZANA NA SIMBA ZATAJWA

SABABU KUBWA ZA KAHATA KUMALIZANA NA SIMBA ZATAJWA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa sababu kubwa ya Francis Kahata kusajiliwa ni uwezo wake mkubwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa pamoja na timu yake ya Gormahia ya Kenya.

Kahata mwenye umri wa miaka 27 leo amemalizana na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili.

Ataungana na kiungo mwenzake Ibrahim Ajibu ambaye naye amejiunga na Simba kwa kandarasi ya miaka mwili kumlisha mipira mchezaji mwenzake wa zamani Meddie Kagere ambaye naye alikuwa mchezaji wa Gormahia.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa usajili wa Kahata ni maalumu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

“Huu ni usajili wa Ligi ya Mabingwa kwa ajili ya TP Mazembe, Al Ahly wakubwa wenzetu,” amesema.

SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED SASA YAMGEUKIA JAMES MADDISSON