Home Uncategorized Yanga sio ‘viti maalumu’, lakini Simba…

Yanga sio ‘viti maalumu’, lakini Simba…

Baada ya taarifa kutoka na kuonyesha kuwa sasa Tanzania itakuwa na timu nne katika mashindano ya CAF, tambwe nyingi zimeenea hadi kupelekea msemaji wa timu ya Simba kutoa maneno ya utani/kejeli kuhusu nafasi hii.

Kandanda imejaribu kuangalia kwa undani kidogo kujua, mchango wa timu hizi ni upi katika kufikisha alama 18 za nchi na kupelekea timu yetu kuinngia nafasi ya 12 na kupata faida ya timu nne (Mbili-Klabu bingwa na Mbili-Kombe la Shirikisho).

Kwa mujibu wa mtandao, Tanzania ipo nafasi ya 12 juu ya Ivory Coast mwenye alama 15 huku Tanzania ikiwa na alama 18. Katika msimu wa 2018/2019 ambapo klabu ya Simba ilifika hatua ya robo fainali ilipata alama 3 hivyo kufikisha alama 15. Hapo kabla ilikuwa na alama 12.


Tunajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha nchi yetu kuingiza timu 4 kwenye michuano ya kimataifa, na tutaendelea kupambana kuhakikisha tunapata mafanikio makubwa kimataifa kwa maslahi ya klabu na nchi yetu. Hongera kwa Wanasimba wote kwa kazi kubwa tuliyofanya, tunastahili pongezi! pic.twitter.com/VpxvpJwKUO

— Mohammed Dewji MO (@moodewji) June 4, 2019


Kwa upande mwingine, Yanga katika ushiriki wake wa mwaka 2016 na 2018 ilipata alama moja (1) tu, ikiwa ni nusu alama kila msimu kwa kutolewa mapema. Hivyo Yanga mpaka sasa ina alama 3 pekee. ukiangalia utofauti wake na Simba, Simba ni kiboko zaidi.

Kwa upande fulani, hizi tambo za mashabiki wa Simba, Yanga inawabidi tu wavumilie. Kwakuwa walitakiwa kufanya vizuri katika miaka yote waliyoshiriki. Na sasa, ndio muda wao labda wa kukimbia ili kujihakikishia wanapata alama nyingi zaidi, lakini ikumbukwe hii si nafasi ya kuteuliwa, ni nguvu ya pamoja kwa miaka mingi.

The post Yanga sio ‘viti maalumu’, lakini Simba… appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  POGBA KUMBE ANAWAZINGUA MANCHESTER UNITED