Home Uncategorized SADNEY AKIWASHA YANGA IKIMPIGA MTU BAO 2-0, MORO

SADNEY AKIWASHA YANGA IKIMPIGA MTU BAO 2-0, MORO

Sadney Urknob leo amekiwasha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Ranger uliochezwa uwanja wa Highland Park kwa kufunga moja ya bao kwenye ushindi wa mabao 2-0.

Leo Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki kwa lengo la kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wakiwa chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.

Sadney alipachika bao hilo dakika ya 38 na bao la pili lilifungwa na Papy Tshishimbi dakika ya 64.

SOMA NA HII  KISA CORONA.. WACHEZAJI WA AZAM FC WATENGWA..!!