Home Uncategorized SIMBA QUEENS WANAPETA TU MAJUU

SIMBA QUEENS WANAPETA TU MAJUU


KIKOSI cha timu ya Simba ya Wanawake, Simba Queens bado kinaendelea na ziara yake ya wiki mbili nchini Ujerumani.

Ziara hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya kujifunza bado inaendelea huku wachezaji wakitembela sehemu mbalimbali kujifunza.

Miongoni mwa sehemu ambazo Simba Queens wamezitembelea ndani ya mji wa Hamburg, Ujerumani ni zile za kihistoria ili waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu utamaduni wa Ujerumani.

Ofisa Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori amesema lengo ni kuimarisha mahusiano na nchi nyingine pamoja na kuitangaza nchi ya Tanzania nje ya nchi.

SOMA NA HII  AZAM FC WABABE WA WACONGO KAZINI LEO FAINALI