Home Uncategorized WEMA SEPETU AMTAJA BINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU UJAO

WEMA SEPETU AMTAJA BINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU UJAO


SHABIKI mkubwa wa timu ya Yanga, Wema Sepetu amesema kuwa ana imani na kikosi cha Yanga kitatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Sepetu amesema kuwa imani yake ni kuona kikosi cha Yanga kinafanya makubwa na anaifuatilia timu yake kwa ukaribu kila hatua.

“Naipenda Yanga na ninaifuatilia katika kila hatua, kwa namna walivyofanya usajili msimu huu,ubingwa unawahusu ni suala la kusubiri tu,” amesema Sepetu.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajili wa na Yanga ni pamoja na Ally Ally, Juma Balinya, Patrick Sibomana, Metacha Mnata.

SOMA NA HII  NZEGELI ATOA KAULI TATA, WAPINZANI TUMBO JOTO