Home Uncategorized ABDI BANDA AANZA MAISHA MAPYA YA SOKA

ABDI BANDA AANZA MAISHA MAPYA YA SOKA


ABDI Banda, nyota wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ baada ya kuitumikia Baroka FC kwa miaka miwili inaelezwa kwa sasa ametua Highlands Park FC ya Afrika Kusini kuanza maisha mapya ya soka.

Baroka FC ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 14, huku Highlands Park ikimaliza ikiwa ya 7 kati ya timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo.

Hivi karibuni Banda aliwaaga viongozi, Wachezaji na mashabiki wa Baroka FC iliyo katika mji wa Polokwane.


“Ninawashukuru mashabiki, viongozi pamoja na benchi la ufundi kwa sapoti ambayo wamekuwa wakinipa na kunifanya niwe na furaha muda wote, kwa sasa nitakuwa sehemu mpya,” amesema.

SOMA NA HII  UTAMU WA LIGI YA MABINGWA HUU HAPA NA MERIDIAN BET