Home Uncategorized BIASHARA UNITED : TUMEJIPANGA KULETA USHINDANI MSIMU UJAO

BIASHARA UNITED : TUMEJIPANGA KULETA USHINDANI MSIMU UJAO


KOCHA wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa msimu ujao ushindani utakuwa mkali hivyo hawatafanya uzembe mwanzoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema kuwa msimu uliopita kulikuwa na ugumu mwishoni kutokana na ushindani uliokuwepo hivyo wanatumia tahadhari hiyo kujipanga.

“Tulikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na ushindani ambao ulikuwepo ila tumejifunza na tumetumia changamoto hiyo kuwa sehemu ya kufanya kitu cha kipekee,” amesema.

SOMA NA HII  BAADA YA UD SONGO, BASI VIZURI MUONYESHE HESHIMA KWA JOHN BOCCO....