Home Uncategorized BALINYA AMWAGIWA NOTI ZA MAANA YANGA, MIFEDHA MINGINE KUTOLEWA

BALINYA AMWAGIWA NOTI ZA MAANA YANGA, MIFEDHA MINGINE KUTOLEWA


Straika wa Yanga, Juma Balinya, juzi alimwagiwa noti za maana na mashabiki wa timu hiyo wanaoishi Bostwana.

Fedha hizo zilitokana na kufunga bao muhimu ambalo liliipa nafasi Yanga ya kuendelea kusalia kunako Ligi ya Mabingwa Afrika.

Balinya aliifungia Yanga bao mnamo dakika ya 42 katika mechi ambayo ilimalizika kwa ushindi wa 1-0 na kuiwezesha kukutana na Zesco United katika mchezo utakaofuata.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, amethibitisha ni kweli Balinya alipokea fedha hizo kutoka kwa mashabiki.

Aidha, Msolla, ameeleza kuwa wamepanga kuwapa fedha wachezaji wote waliokuwa kwenye msafara kama motisha na yote hii inachagizwa na ushindi wa juzi.

SOMA NA HII  PATRICK GAKUMBA AFUNGUKA JUU YA BALINYA KUTOENDA SIMBA 'WALIMKATAA' - VIDEO