Home Uncategorized BIASHARA UNITED YAIPIGIA HESABU ZA MBALI KAGEA SUGAR

BIASHARA UNITED YAIPIGIA HESABU ZA MBALI KAGEA SUGAR



UONGOZI wa Biashara United umesema kuwa kazi kubwa kwa sasa wanaiwekeza kuandaa kikosi kitakacholeta ushindani msimu ujao.

Amri Said Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa mchezo wake wa kwanza dhidi ya Kager Sugar utakuwa ni wa kukata na shoka kutokana na maandalizi ya timu zote mbili.

Agosti 24, Biashara United itafungua panzia na Kagera Sugar uwanja wa Karume, Mara na utakuwa ni mchezo wao wa kwanza kuanzia nyumbani kwa msimu mpya wa 2019/20.

Akizungumza na Salehjembe, Said amesema amekiandaa kikosi Kwa namna ya kipekee anaimani ya kuibuka na ushindi. 


“Mchezo wetu wa kwanza ni muhimu kupata ushindi, tumejipanga kufanya vizuri na tupo tayari kwa ushindani. 

“Haitakuwa rahisi kupata matokeo chanya haraka mbele ya wapinzani wetu ukizingatia kila timu imejipanga, ni jambo la kusubiri na kuona namna tutakavyopambana kutafuta matokeo,” amesema.

SOMA NA HII  ASTON VILLA KWENYE MTIHANI MGUMU LEO MBELE YA ARSENAL