Home Uncategorized ASTON VILLA KWENYE MTIHANI MGUMU LEO MBELE YA ARSENAL

ASTON VILLA KWENYE MTIHANI MGUMU LEO MBELE YA ARSENAL


ASTON Villa anakokipiga nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania,  Mbwana Sammatta leo ina kibarua cha kupambania kufufua matumaini ya kubaki ndani ya Ligi Kuu England msimu wa 2020/21.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Villa Park leo Julai 21 majira ya saa nne usiku  umeshikilia hatma ya Villa ambayo ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 36.

Ikiwa Villa itashinda mchezo wa leo itafikisha pointi 34 huku ikiwaombea wapinzani wao Bournemouth kupoteza mchezo wao dhidi ya Everton unaotarajiwa kuchezwa Julai 25.

Kazi ya mwisho kwa Villa itakuwa ni kusaka ushindi wa aina yoyote mchezo wake mbele ya West Ham United ambapo itakuwa ugenini Julai 26 ili kujihakikishia nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu England. 

Arsenal iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 53 baada ya kucheza mechi 36.

SOMA NA HII  KAZE ABAINISHA MKAKATI NAMBA MOJA WA YANGA