Home Uncategorized MEDDIE KAGERE ATAJA SIRI YA KUFUNGA MABAO 22 NDANI YA LIGI

MEDDIE KAGERE ATAJA SIRI YA KUFUNGA MABAO 22 NDANI YA LIGI


MEDDIE Kagere,mtupiaji namba moja ndani ya Simba amesema kuwa siri kubwa ya mafanikio yake ya kucheka na nyavu ni kumuomba Mungu na kufanya kazi kwa juhudi ndani ya uwanja.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kagere amesema kuwa hesabu kubwa ni kuona anafikia malengo aliyojiwekea na kufanya kazi bila kukata tamaa.

“Kwangu mimi ninajua kwamba siri ya mafanikio ni Mungu kwani nimekuwa nikimuomba kila wakati na mimi pia ninaongeza juhudi katika kazi yangu.

“Ushirikiano ambao ninapewa na wachezaji wenzangu unanifanya ninakuwa katika kiwango ambacho nipo nacho kwa sasa na wakati ujao pia.

“Ninajua kuwa tuna mchezo dhidi ya Coastal Union bado tunaendelea kujiandaa ili kufanya vizuri mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Kagere raia wa Rwanda ni kinara kwa upande wa utupiaji akiwa ametupia jumla ya mabao 22 na kutoa pasi sita za mabao.

Anafuatiwa kwa ukaribu na mzawa, Yusuph Mhilu mwenye mabao 13 akiwa ndani ya Kagera Sugar.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo na imeshatwaa ubingwa wa ligi kibindoni ina pointi 84 na imefunga jumla ya mabao 76.

SOMA NA HII  LIGT AUNGANA NA CR7 JUVENTUS, ASAINI MIAKA MITANO