Home Uncategorized KOCHA TANZANITE: TUPO TAYARI KUWAVAA ESWATINI LEO

KOCHA TANZANITE: TUPO TAYARI KUWAVAA ESWATINI LEO


BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania chini ya miaka 20,’Tanzanite’ amesema kuwa leo kikosi kipo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya mbele ya Eswatini leo.

Tanzanite wamealikwa kwenye michuano hiyo inayofanyika nchini Afrika Kusini na mchezo wa kwanza ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Botswana.

Leo wanashuka uwanjani kumenyana na Eswatini mchezo wao wa pili utakaochezwa Uwanja wa Gelvaland.

“Mchezo wa kwanza mbinu zetu zilikuwa hazijulikani kwa wapinzani ila kwa sasa tayari wameshazitambua hilo halitupi wasiwasi kwani tumejipanga kufanya vizuri.

“Mchezo wetu wa kwanza wachezaji walikuwa na wasiwasi licha ya kushinda ila kwa sasa morali imeongezeka na kila kitu kinakwenda sawa,” amesema.

SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO NDANI YA AZAM FC KAZINI TENA LEO