Home Uncategorized KUMEKUCHA! YANGA WATUPA DONGO KIMTINDO KWA SIMBA

KUMEKUCHA! YANGA WATUPA DONGO KIMTINDO KWA SIMBA


UONGOZI wa Yanga umeamua kutupa dongo kimtindo kwa wapinzani wao Simba kuhusu ubora wa jezi zao.

Kwa sasa vita kubwa iliyopo ni nani ana jezi bora huku kila timu kati ya Simba na Yanga zikivutia kamba kwao kuonyesha kwamba ubora wao ni wa hali ya juu.

Dismas Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa wapinzani wao wanatambua kuwa Yanga wana jezi bora na wanapenda kuzinunua ila wamekuwa wakizikosa madukani.

” Wapinzani wetu wanajua kwamba tuna jezi nzuri na wao wanapenda kuzivaa ila wanazikosa hivyo kwa sasa tumejipanga kuona kwamba zinapatikana kila kona.

“Kwa sasa ni suala la mashabiki wetu wa Yanga kutafuta jezi halisi kwenye maduka yetu ya GSM huko watapata jezi nzuri mfano wake hakuna,” amesema.

SOMA NA HII  SENZO AMKATALIA SVEN, MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU