Home Uncategorized MKAKATI MKUBWA WA AZAM FC KUINYOOSHA SIMBA JUMATANO UMEJIFICHA KWA HAWA

MKAKATI MKUBWA WA AZAM FC KUINYOOSHA SIMBA JUMATANO UMEJIFICHA KWA HAWA


UONGOZI wa Azam FC umewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa, Jumatano ya Machi 4 kuipa sapoti timu hiyo itakapomenyana na Simba ili kuwapa nguvu ya kushinda mbele ya wapinzani hao.

Mchezo huo utakuwa wa pili wa ligi ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere kwa kichwa akimalizia pasi ya Francis Kahata.Utachezwa majira ya saa 1:00 usiku.

Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa miongoni mwa nguzo muhimu kwa timu ni mashabiki hivyo kujitokeza kwao kwenye mechi kunawapa nguvu ya kupambana.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA KMC DHIDI YA AS KIGALI HIKI HAPA