Home Uncategorized KUMBE SAKATA LA KICHUYA SIMBA WENYEWE WAMEHUSIKA

KUMBE SAKATA LA KICHUYA SIMBA WENYEWE WAMEHUSIKA


 BAADA ya kuelezwa kuwa kiungo mshambuliaji Mtanzania Shiza Kichuya amefungiwa kutocheza soka kwa muda wa miezi sita na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baba mzazi wa kiungo huyo, Ramadhan Kichuya ameitupia lawama Simba kwa kushindwa kukamilisha taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo.

 

Kichuya alishitakiwa na klabu yake ya zamani ya Pharco ya Misri iliyomsajili mwaka 2019, kabla ya Januari mwaka huu kuibukia Simba na sasa anaichezea Namungo FC ya Lindi.

 

Wakati Kichuya akikutana na kifungo hicho Simba wao wamepigwa faini ya Dola 130,000 sawa na Sh 300m.


Baba Kichuya amesema:-“Awali Simba walimwambia kuwa aje Tanzania wao watamaliza taratibu zote lakini imekuwa tofauti.

 

“Makosa ya klabu ndiyo yanayosababisha matatizo kama hayo, ukichukulia mfano wale viongozi wa Simba walishamchoka kwa sababu walisema kiwango chake kilishuka mpaka kufikia muda wakampeleka kwa mkopo Namungo.

 

“Mimi naona hawatendi haki, wamesahau vile walikuwa wanamtegemea zamani.


 “Ila namuombea Mungu miezi hiyo iishe na arudi kwenye soka kwani ana kipaji na siyo cha kulazimisha,” alisema baba Kichuya.

 

Aidha, Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hemed Morocco naye alisema kukosekana kwa mchezaji huyo ni pigo kwa timu hiyo ambayo itashiriki michuano ya kimataifa.


Chanzo Championi

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA MWADUI FC, MANULA NJE