Home Uncategorized KUMEKUCHA HUKO JANGWANI, FUNGU LA KUTOSHA LAWEKWA MEZANI KUIMALIZA SIMBA

KUMEKUCHA HUKO JANGWANI, FUNGU LA KUTOSHA LAWEKWA MEZANI KUIMALIZA SIMBA


 KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi, Yanga na Simba unaotarajiwa kuchezwa, Machi 8, Uwanja wa Taifa tayari mkwanja umewekwa mezani ili Yanga imalize mchezo huo mapema.

Imeelezwa kuwa miongoni mwa wadhamini wa Yanga, Kampuni ya GSM, imeweka mezani mamilioni ya fedha endapo Yanga itashinda mchezo huo kwa idadi yoyote ya mabao.

“Mchezo wa kwanza wachezaji waliwekewa mezani milioni mia mbili ila Ile sare ya kufungana mabao 2-2 waliambulia milioni 50 lakini safari hii mkwanja umeongezeka iwapo watashinda.

“Kinachoendelea kwa sasa ni hamasa na kuona namna gani wachezaji watapata ushindi mbele ya Simba, wameahidi kufa na kupona ili kupata mkwanja na pointi tatu,” kilieleza chanzo hicho.
SOMA NA HII  DI MARIA ALIWAKA KWELI WAKATI PSG IKITINGA HATUA YA FAINALI