Home Habari za Simba Leo SABABU ZA KIBU DENIS KUTOENDA MISRI.

SABABU ZA KIBU DENIS KUTOENDA MISRI.

Habari za Simba SC

WAKATI Willy Onana na nyota mpya aliyetambulishwa hivi karibuni, Awesu Awesu jana walipaa kwenda kuongeza mzuka katika kambi ya Simba iliyopo, Ismailia Misri, nyota wa timu hiyo, Kibu Denis amezua utata.

Awesu na Onana ni kati ya wachezaji waliondoka nchini juzi sambamba na baadhi ya viongozi kwenda Misri kuungana na wachezaji wengine wanaoendelea kujifua chini ya kocha mpya Fadlu Davids, lakini Kibu akiwa haonekani kambini na taarifa ni bado yupo Marekani akiendelea kula zake bata na familia.

Inaelezwa kwamba Winga wa Simba Kibu Denis aliyekuwa mapumzikoni Marekani, tatizo lililomfanya ashindwe kujiunga na timu kwa wakati ni kutokana na changamoto ya VISA ya kusafiria.

Visa ya Kibu Denis aliyepewa uraia wa Tanzania, ilikuwa na matatizo hivyo kukwamisha yeye kujiunga na wenzake huko Misri, lakini jitihada za kuhakikisha jambo linakamilika harakazilifanyika na hivi sasa kila kitu kipo tayari.

Hadi wakati huu Kibu Denis yupo Dar na ataondoka haraka kwenda Ismailia Misri kujiunga na wenzake.

Tangu Simba iweke kambi nchini humo hii ni wiki ya pili inaanza, huku hali ya kambi ya Simba ikiripotiwa kuwa ni shwari kila kitu kinaenda kama kilivyopagwa.

Hadi wakati huu ikiwa imesalia siku moja kufungwa kwa dirisha la usajili la CAF, Simba imeshasajili wachezaji 27 huku dili la Mpanzu likionekana kuota mbawa.

SOMA NA HII  CHAMA : MSIMU HUU TUNAKUJA NA STAILI YA MANDONGA...ITAKUWA AIBU KUBWA SANA KWA SIMBA....