Home Habari za Yanga Leo UKWELI KUHUSU SUALA LA JEAN BALEKE YANGA

UKWELI KUHUSU SUALA LA JEAN BALEKE YANGA

Habari za Yanga- baleke

Kumekuwa na maswali mengi juu ya kushindwa kutambulishwa kwa Jean Baleke licha ya straika huyo wa zamani wa Simba kuonekana mazoezini na kuwa kwenye msafara wa Yanga unaoenda Afrika Kusini na Mwanaspoti likajaribu kuchimba kujua ukweli.

Inaelezwa pamoja na Baleke kupewa mkataba wa mwaka mmoja na Yanga, pia bado ni mchezaji wa TP Mazembe, hivyo klabu zinazomhitaji lazima zizungumze na wahusika, hata hivyo Yanga imemalizana na klabu hiyo ya DR Congo, lakini tatizo lipo kwa Al Ittihad ya Libya aliyokuwa akiitumikia kwa mkopo.

Tunafahamu kwamba Baleke, alibakiza mkataba wa miezi sita na Al Ittihad, kwani alisaini mwaka mmoja na ametumikia nusu, hivyo inawia ngumu Yanga kutangaza kwa sababu itaonekana imesajili mchezaji wa klabu nyingine na itaingia kwenye mgogoro na Walibya.

Chanzo cha taarifa hiyo kinasema, “Yanga tumemalizana na TP Mazembe, ishu inakuja timu aliyotokea ndio tunashughulikia hilo, ili tuwe huru na mchezaji wetu. Ndio maana amerudishwa Kennedy Musonda ambaye tulikuwa na lengo la kuachana naye, lakini nisisitize tunaendelea kulishulikia.”

Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kupita Simba na kufunga jumla ya mabao 16 kwa msimu mmoja na nusu, amekuwa akionekana katika uwanja wa mazoezi na klabu ya Yanga.

Lakini  pia ni sehemu ya wachezaji waliosafiri kwenda Afrika Kusini kwenye mechi za Kirafiki dhidi ya FC Augsburg ya Ujerumani.

SOMA NA HII  WINGA HUYU HATARI ATHIBITISHA KUSAJILIWA NA SIMBA...