Home Habari za Simba Leo WADAU WAMPIKA BALEKE…CHANZO KWENDA YANGA.

WADAU WAMPIKA BALEKE…CHANZO KWENDA YANGA.

Baleke to Yanga

ALIYEKUWA Mshambuliaji wa Simba SC Jean Baleke ambaye ameonekana kwa nyakati tofauti na Yanga, amezua maswali mengi na ukosaoji mwingi kutoka kwa wadau wa soka ikiwemo Steve Mapunda Garrincha.

Baleke ambaye aliondoka Simba na kujiunga na Al Ittihad ya Libya, katika dirisha dogo alikuwa mfungaji bora wa Ligi hiyo na sasa bado ana mkataba wa mkopo na klabu hiyo.

Lakini licha ya mkopo wake ambao haumzuii yeye kusajiliwa na timu nyingine, ameonekana akiwa katika mazoezi ya Yanga Avic Town, na Gym Khana pamoja na fukwe na Coco Jiji Dar Es Salaam.

Hata leo wakati timu hiyo ikisafiri kwenda Afrika Kusini kwenye mualiko wa mechi za kirafiki dhidi ya Kaizer Chief na FC Augsburg ya Ujerumani, Baleke alionekana kwenye msafara wa mastaa kibao wa Yanga ukiongozwa na Clatous Chama.

Staa wa zamani wa Simba, Steven Mapunda ‘Garrincha’ amesema japo Simba, imesajili vizuri, hapendezewi kuona mshambuliaji kama Baleke anakuwa upande wa upinzani.

“Silaha inapokwenda kwa mpinzani, maana yake unajiongezea ugumu wa vita, ingawa katika usajili uliofanywa nayaona malengo makubwa ya Simba msimu ujao na mingine mbele,” alisema nyota huyo wa kimataifa aliyewahi kuwika pia na Majimaji na Taifa Stars.

Akizungumiza kukutana kwa baadhi ya wachezaji wa Simba na Yanga kwenye mchezo ujao wa kufungua mbio za Ligi Kuu ya NBC, msimu wa 2024/25.

Kwa upande kipa wa zamani wa Yanga, Benjamin Haule amesema; “Itakuwa mechi ngumu, kwani timu hizo zimefanya maboresho ya vikosi vyao.”

Beki mwingine wa zamani wa klabu hizo, Amiri Maftah amesema; “Simba na Yanga hazina shoo ndogo, najua utakuwa mchezo mgumu yoyote anaweza akatoka na ushindi bila kujali nani yupo vizuri ama vibaya.”

SOMA NA HII  HIZI HAPA HESABU ZA SIMBA DHIDI YA POWER DYNAMOS