Home Habari za Simba Leo DILI LA MPANZU SIMBA LAOTA MBAWA…ONANA ARUDISHWA KUNDINI

DILI LA MPANZU SIMBA LAOTA MBAWA…ONANA ARUDISHWA KUNDINI

Habari za Simba- Elie Mpanzu

DILI la Winga wa Kimataifa wa DR Congo Elie Mpanzu kujiunga na Simba kwa msimu ujao 2024/25 limeota mbawa rasmi kutokana na ugumu uliowekwa kutoka klabu ya AS Vita.

Rais wa Klabu hiyo Amadou Diaby aliingilia kati dili hilo na Kumshawishi Elie Mpanzu Kibisawala aendelee kubaki ndani ya timu hiyo kwa kumuahidi kumpatia mshahara mkubwa zaidi.

Winga huyo ni miongoni mwa wachezaji waliohitajika na Simba katika dirisha hili la usajili ili kuboresha kikosi hicho ambacho kinajengwa upya ili kuleta ushindani msimu ujao baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo.

Inanelezwa kwamba Elie Mpanzu alishawaaga hadi wachezaji wa timu hiyo huku akiwaambia anataka kupata changamoto sehemu nyingine jambo ambalo lilimfanya Amadou kufanya kikao cha siri na mchezaji huyo.

Katika kikao hicho inaelezwa ndicho kilichobadilisha upepo na Winga huyo kujiunga na Simba, ambapo inaelezwa ameongezewa mkataba wa miaka mitatu zaidi na mshahara mkubwa tu, huku wakifikiria kumpa kitambaa cha Unahodha yote hayo ni kumshawishi mchezaji kujiona wa thamani kubwa klabuni hapo.

Mjumbe mmoja wa Simba Salim Abdallah alifikia kwenda hadi Kinshasha CONGO kwaajili ya kujaribu kuweka mabo sawa, ya kumpata Elie Mpanzu.

“Ni kweli Try Again yupo Congo, lakini siwezi kusema kwamba ameenda kwa ajili ya dili hilo kwa sababu huwa ni mtu ambaye anaenda nchi mbalimbali kwa mambo yake binafsi. Kama ni hivyo sawa ila siwezi kukuhakikishia,” kimesema chanzo kutoka ndani ya Simba.

Hata hivyo, wakati AS Vita ikimbakiza nyota huyo, lakini uongozi wa timu hiyo tayari umeanza kutafuta mbadala wake huku ikielezwa inahitaji kumrejesha aliyekuwa winga wa kikosi hicho, Marouf Tchakei.

AS Vita inapiga hesabu za kumrudisha Tchakei ambaye kabla ya kutua nchini alitokea timu hiyo na kujiunga na Singida Big Stars na baadaye Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars kuanzia Julai Mosi, mwaka jana.

SOMA NA HII  KISA PESA ZA WAARABU....ISHU YA INONGA NA SIMBA NGOMA BADO NGUMU...