Home Uncategorized NEEMA YAZIDI KUMIMINIKA NDANI YA YANGA

NEEMA YAZIDI KUMIMINIKA NDANI YA YANGA

NEEMA imezidi kumiminika ndani ya uongozi wa Yanga baada ya mlinzi wa zamani wa Yanga, Ahmed Amasha kuukabidhi uongozi wa timu hiyo vifaa mbalimbali vya mazoezi.

Amasha aliyeitumikia Yanga kati ya mwaka 1980 na 1985, amekuwa na utaratibu wa kutoa misaada mbalimbali kwa klabu hiyo.

Amasha kwa sasa anaishi Arabuni, amewataka wadau wengine wa Yanga ambao wanaishi nje ya nchi wasiisahau timu yao.

“Ni wakati wa wadau na mashabiki wenye mapenzi na Yanga kuwekeza ndani ya klabu hii kwa manufaa ya timu hapo baadaye kwani nafasi ni sasa na kila kitu kinawezekana,” amesema.

SOMA NA HII  LIST KAMILI YA WACHEZAJI SIMBA WATAKAOIKOSA UD SONGO LEO HII HAPA - VIDEO