Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAFICHUA KILICHO NYUMA YA USHINDI WAO LEO MBELE YA YANGA

RUVU SHOOTING YAFICHUA KILICHO NYUMA YA USHINDI WAO LEO MBELE YA YANGA


SADAT Mohamed, mshambuliaji wa Ruvu Shooting amesema kuwa amefurahi kuipa ushindi leo timu yake ya Ruvu Shooting mbele ya mabingwa wa kihitoria Yanga.

Akizungumza mara baada ya mchezo, Mohamed amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kufikia hapo kutokana na ushindani mkubwa ambao ulikuwepo kwenye mchezo wa leo.

“Tumepambana mwanzo mwisho na mchezo ulikuwa mgumu mwisho wa siku tumepata ushindi na pointi tatu kwetu ni jambo la msingi na la furaha sana.

“Ushirikiano ambao tumekuwa tukiufanya na namna ya mazoezi ambayo tumeyafanya yametusaidia kutupa ushindi mbele ya Yanga leo tutazidi kupambana na siri ya ushindi ipo kwenye ushirikiano,” amesema.

Ruvu Shooting msimu uliopita ilipigwa na Yanga nje ndani leo ni mara ya kwanza kusepa na pointi tatu mbele ya Yanga uwanja wa Uhuru.

SOMA NA HII  YANGA WAMKOMALIA MORRISON, LENGO LAO KWENDA CAS LIPO PALEPALE