Home Uncategorized SERIKALI YAIKUBALI YANGA, YAHOJI NANI ANAYESEMA NI DHAIFU

SERIKALI YAIKUBALI YANGA, YAHOJI NANI ANAYESEMA NI DHAIFU


JERRY Muro, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani ambaye aliwahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga amewashangaa wanaodai kuwa Yanga ni timu dhaifu.

Muro amesema: “Nani anasema Yanga ni timu dhaifu? Yanga ni timu Bora msimu huu kuliko timu yoyote isipimwe uwezo wake kwa mechi za kirafiki itakuja kufanya balaa siku za usoni,” amesema.

Yanga ilipoteza hivi karibuni mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania uliochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi Kwa kufungwa mabao 2-0 ambapo wafungaji walikuwa ni Marcel Kaheza na Ditram Nchimbi.


Mwinyi Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kushindwa kufurukuta mbele ya Polisi Tanzania ni ubovu wa Uwanja.

SOMA NA HII  BREAKING :NIYONZIMA ASAINI AZAM FC, KILICHOWASHINDA YANGA CHATAJWA