Home Uncategorized SERIKALI YAIPA TANO ZA KUTOSHA TANZANITE

SERIKALI YAIPA TANO ZA KUTOSHA TANZANITE


NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Juliana Shonza amesema kuwa mafanikio ya timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ ni matokeo ya uwekezaji kwenye mpira.

Tanzanite kwa sasa wapo jijini Dar, baada ya kutoka kupeperusha Bendera ya Taifa nchini Afrika Kusini kwenye michuano ya COSAFA na wamerejea na kombe hilo licha ya kualikwa.

Shonza amesema: “Wachezaji wetu wameonyesha namna uwekezaji unavyotoa matokeo chanya pamoja na kupeperusha Bendera kwa kujiamini ugenini ni jambo ambalo wanastahili pongezi.

“Kufanya kwao vizuri ni kitu cha kujivunia kwa Taifa kwani licha ya kualikwa wamerejea na kombe, lengo la Serikali ni kuona kila siku tunafikia yale malengo ambayo tunajiwekea, TFF pamoja na wadau ni muda wa kuwekeza kwa ajili ya baadaye,” amesema.

SOMA NA HII  HAWA IHEFU WATOE DARASA KWA WAKONGWE NAMNA YA KUJIJENGA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU