Home Uncategorized SIMBA YAZIDI KUIPOTEZA MAZIMA YANGA, MO AONGEZA MABILIONI MENGINE KIKOSINI

SIMBA YAZIDI KUIPOTEZA MAZIMA YANGA, MO AONGEZA MABILIONI MENGINE KIKOSINI


Mfanyabiashara Bilionea na Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji Mo, ameongeza bajeti ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita mara mbili na nusu kutoka bilioni 1-3, imeelezwa.

Kwa msimu uliopita bajei ya Simba iliyosaidia kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilitumia bilioni 1.3 zilizosaidia pia kutwaa ubingwa wa ligi.

Ongezeko la bajeti hiyo kubwa kutoka kwa Mo limekuja kufuatia kufanya vizuri kwa Simba huku Mwekezaji huyo akionesha kufurahishwa na timu yake.

Taarifa zinasema wakati akizungumza na kituo cha Radio BBC kurtoka London, Uingereza, Mo amefunguka kuwa sehemu ya mafanikio ambayo Simba imeyapata kwa msimu yamechangia kuongezeka kwa bajeti.

Aidha, ameeleza kuwa kwa sasa Simba haina haja ya kufanya matangazo makubwa ya kuwaita mashabiki na badala yake watakuwa wanaenda wao uwanjani kufuatia ubora wa kikosi ambacho wanacho.

SOMA NA HII  MBEBA MIKOBA YA JONAS MKUDE, MAJANGA MATUPU