Home Uncategorized WALIOOA FC WACHEKELEA SAPOTI YA SALEH JEMBE

WALIOOA FC WACHEKELEA SAPOTI YA SALEH JEMBE


NAHODHA wa timu ya Waliooa FC wa Kampuni ya Global Group Publisher, Philip Nkini amechekelea udhamini wa nguvu kutoka kwa Saleh Jembe.

Waliooa FC wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na wale ambao hawajaooa Ijumaa ya wiki ijayo.

Nkini amesema kuwa sapoti kubwa ambayo wameipata kutoka kwa Saleh Jembe ambayo ni ya kambi, malazi na chakula vitawapa nguvu ya kuwanyoosha wapinzani wao.

“Tunashukuru kwa udhamini mkubwa ambao tumeupata kutoka kwa Saleh Jembe, ni muda wetu kujipanga na kufanya makubwa kuonyesha thamani ya udhamini wake,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA HAWAPOI WAJIBU DONGO LA SIMBA KWA VITENDO, CHEKI JIBU LAO LAZIMA UKAE