Home Uncategorized REKODI HII YA KASEJA NDANI YA TAIFA STARS NA MWENZAKE WA BURUNDI...

REKODI HII YA KASEJA NDANI YA TAIFA STARS NA MWENZAKE WA BURUNDI NOMA SANA


JUMA Kaseja mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania ametoshana nguvu na Jonathan Nahimana mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Burundi Kwa wote wawili kukubali kufungwa bao mojamoja.

Nyota hao wote walikaa langoni kwa muda wa dakika 90 na wanakipiga pamoja kwenye timu ya KMC yenye maskani yake Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Kwanza wa kuwania Kombe la Dunia litakalofanyika mwaka 2022 nchini Qatar ulichezwa Uwanja wa Prince Louis Rwagasore.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika Septemba 8 Uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  JONAS MKUDE AWAPOTEZA WOTE NDANI YA SIMBA