Home Uncategorized BAADA YA KUITUNGUA YANGA, MTIBWA SUGAR YAIPIGA MKWARA MZITO SIMBA

BAADA YA KUITUNGUA YANGA, MTIBWA SUGAR YAIPIGA MKWARA MZITO SIMBA



KESHO, Visiwani Zanzibar, Uwanja wa Amaan, kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati a Mtibwa Sugar na Simba ambao utakuwa ni wa fainali ya Kombe la Mapinduzi.


Mtibwa Sugar walikuwa wa kwanza kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa penalti 4-2 walioupata mbele ya Yanga baada ya dakika tisini kulazimisha sare ya bao 1-1.

Simba nao walikuwa washindi wa nusu fainali ya pili mbele ya Azam FC kwa ushindi wa penalti 3-2 baada ya dakika tisini kutoka sare ya bila kufungana.

Azam FC ambao walikuwa mabingwa watetezi msimu huu watakuwa watazamaji wa fainali hii itakayopigwa Januari,13.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na timu zote kupania kutwaa taji la kwanza kwa mwaka 2020.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Humud amesema kuwa mchezo mgumu ulikuwa dhidi ya Yanga wana imani watapenya mbele ya Simba na kupata matokeo.

Kwa upande wa Simba, mlinda mlango, Beno Kakolanya amesema kuwa wachezaji wapo vizuri na wanaamini utakuwa mchezo mgumu ila watapabana kupata matokeo.
SOMA NA HII  SENEGAL WAPATA PIGO LEO KUMKOSA BEKI WAO KISIKI FAINALI YA AFCON