Home Uncategorized BOSI SIMBA AFUNGUKA JUU YA KUACHANA NA NYOTA TEGEMEO

BOSI SIMBA AFUNGUKA JUU YA KUACHANA NA NYOTA TEGEMEO


Uongozi wa klabu ya Simba umesema haujaachana na wachezaji wake Aishi Manula pamoja na Erasto Nyoni.

Kwa mujibu wa CEO mpya wa Simba, Senzo Mazingisa, ameeleza kuwa si kweli wameachana na wachezaji hao baada ya kuwa kwenye majeruhi hivi karibuni.

Akizungumza na Radio One, Mazingisa ameeleza bado wachezaji hao ni mali halali ya Simba na wataendelea kuwa nao siku zote.

Amefunguka kuwa wanaheshimu mchango wao na yanayoelezwa mitandaoni kuwa wameachana nao hayana ukweli wowote.

“Nyoni na Manula ni wachezaji wa Simba, hatujaachana nao kama inavyoelezwa.

“Sisi tutaendelea kuwa nao sababu kuwa majeruhi si chanzo cha sisi kuachana nao, yanayoandikwa yapuuzwe.”
SOMA NA HII  VIKOSI VIWILI VYA YANGA ACHA KABISA,MUGALU ATOWEKA SIMBA,NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO