Home Uncategorized SITA WAPIGWA CHINI JUMLA NDANI YA KMC

SITA WAPIGWA CHINI JUMLA NDANI YA KMC


IMEELEZWA kuwa Uongozi wa timu ya KMC umefikia makubaliano ya kusitisha mikataba na wachezaji watano ndani ya kikosi hicho.

Wachezaji hao ni Aaron Lulambo, George Sangija, Rehani Kibingu, Melly Mongolare na Janvier Besala Bokongu.

Pia mchezaji Vitalis Mayanga ameuzwa kwa timu ya Ndanda FC ya Mtwara ambako ndiko alikotoka kabla ya kusajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili ndani ya KMC.


Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa iliyofanya haya yote kutokea ni wachezaji kushindwa kuonyesha uwezo wao ndani ya uwanja.
SOMA NA HII  HAWA HAPA MAPILATO WA LEO KWENYE MCHEZO WA ROBO FAINALI KATI YA SIMBA NA AZAM FC TAIFA