Home Uncategorized YANGA: TUTAREJESHA FURAHA ILIYOPOTEA

YANGA: TUTAREJESHA FURAHA ILIYOPOTEA


 ANTONIO Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga amesema leo timu yao itapambana kupata matokeo chanya mbele ya Singida United.

Yanga iliyo chini ya Mbelgiji, Luc Eymael ilipoteza mechi mbili mfululizo kwa kuchapwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Azam FC, leo itamenyana na Singida United, Uwanja wa Namfua.

“Hatujawa na mwendo mzuri hivi karibuni ni jambo la kusikitisha ila haina maana tunapaswa tukate tamaa, tutapambana mbele ya Singida United kurejesha furaha iliyopotea,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 25 kibindoni baada ya kucheza mechi 14.

SOMA NA HII  WACHEZAJI LIGI KUU BARA WAPEWA DARASA NAMNA YA KULINDA VIPAJI VYAO