GERALD Mdamu, mshambuliji wa Mwadui FC amesema kuwa wachezaji wana morali ya kupambana mbele ya Mbao FC mchezo utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Mdamu ametupia jumla ya mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa wachezaji wamekubaliana kupambana ili kupata matokeo mazuri yatakayowatoa kwenye nafasi ambayo wapo kwa sasa.
“Ligi imekuwa na ushindani mkubwa kwa sasa tumelitambua hilo, mbinu ambazo tumepewa na mwalimu tutazitumia na tutapambana ili kupata pointi tatu muhimu,” amesema.
Mwadui FC ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo ikiwa na pointi 19 ilizojikusanyia kibindoni.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.