Home Uncategorized ALIYEMPIGA TEKE MWAMUZI YAMKUTA, TFF YALA NAYE SAHANI MOJA

ALIYEMPIGA TEKE MWAMUZI YAMKUTA, TFF YALA NAYE SAHANI MOJA

Habari za michezo
Mechi namba 80 Gipco FC 1 vs Gwambina FC 2- Meneja wa timu ya Gipco Ayubu Msonge amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga teke mwamuzi wa mchezo huo tajwa baada ya mchezo kumalizika pindi waamuzi walipokuwa wanatoka uwanjani, kitendo hicho kilifanyika February 08, 2020 katika uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.
Klabu ya Gipco imetozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) kutokana na timu hiyo kushindwa kuhakikisha usalama kwenye mchezo uliofanyika February 08, 2020 katika uwanja wa Nyankumbu ikiwa ni jukumu lao kama timu mwenyeji, hivyo kutokea vurugu zilizosababisha kupigwa kwa afisa wa Bodi ya Ligi na waamuzi wa mchezo huo tajwa katika uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43 (1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Uthibiti wa Klabu.
Kamati imeieleza timu ya Gipco FC kuwa endapo vitendo hivyo vitajirudia tena katika mchezo mwingine watakaocheza, haitasita kuchukua maamuzi makubwa zaidi ikiwemo kuwabadilishia uwanja wa nyumbani wa klabu yako (home ground) na kupangiwa uwanja mwingine.

Mechi namba 78- Transit Camp FC 4 vs Mawenzi FC 0– Meneja wa timu ya Mawenzi Fc Christopher Mapunda amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kutoa lugha za matusi katika mchezo huo tajwa uliofanyika February 2, 2020 katika uwanja wa Uhuru jjini Dar es Salaam.
SOMA NA HII  LIPULI: TUNAIPIGA AZAM FC NA PIPA TUNAKWEA