Home Uncategorized HIKI NDCHO KINACHOMPA KIBURI EYMAEL KUSEPA NA POINTI TATU ZA MBEYA CITY

HIKI NDCHO KINACHOMPA KIBURI EYMAEL KUSEPA NA POINTI TATU ZA MBEYA CITY


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anaamini kwa maandalizi waliyoyafanya leo watapata pointi tatu mbele ya Mbeya City.

Yanga itamenyana na Mbeya City leo mchezo wa Ligi Kuu Bara, utakaopigwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa uwezo wa wachezaji wake umekuwa ukiongezeka kila siku jambo linalompa matumaini.

“Utofauti upo na ninaona kila siku maendeleo ya wachezaji wangu, kikubwa ninachoamini ni wachezaji wangu kupambana na kutafuta pointi tatu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 ikiwa na pointi 37.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO