Home Uncategorized HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOBANANA NA POLISI TANZANIA USHIRIKA MOSHI JANA

HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOBANANA NA POLISI TANZANIA USHIRIKA MOSHI JANA

YANGA Jana ikiwa ugenini mbele ya Polisi Tanzania ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi.
Licha ya Yanga kuanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 41 kupitia kwa Tariq Seif kwa kichwa akimalizia pasi ya Bernard Morisson na kuwapeleka Polisi Tanzania iliyo chini ya Malale Hamsini mapumziko ikiwa nyuma kwa bao hilo halikudumu.
Polisi Tanzania walisubiri mpaka dakika ya 61 ambapo Sixtus Sabilo alichonga krosi iliyokutana na kichwa cha Matheo Anthon na kukizamisha nyavuni, mwamuzi alikataa hilo bao baada ya kujadiliana na mshika kibendera.
Wachezaji wa Polisi Tanzania wakiongozwa na nahodha wao Idd Moby walitulia na kurejea mchezoni dakika saba mbele walisawazisha bao hilo dakika ya 71 kwa kichwa kupitia kwa Sixtus Sabilo aliyefunga bao kwa kichwa akimalizia pasi ya Marcel Kaheza.
Sare hii inakuwa ni ya tatu mfululizo kwa Yanga iliyo chini ya Mbelgiji, Luc Eymael alianza kupata sare ya kufungana bao 1-1 na Mbeya City kisha ikafuata ya bila kufungana na Prisons zote Uwanja wa Taifa na jana mbele ya Polisi Tanzania.
Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 inafikisha jumla ya pointi 40 ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo na inafikisha jumla ya sare saba ikiwa imeshinda mechi 11 na kupoteza mechi tatu.

SOMA NA HII  NYOTA WAPYA SIMBA WAANZA MATIZI, MORRISON KAMA KAWAIDA HAISHIWI JAMBO