Home Uncategorized KAGERE ATAJA KINACHOMBEBA NDANI YA SIMBA

KAGERE ATAJA KINACHOMBEBA NDANI YA SIMBA


MEDDIE Kagere amesema kuwa kikubwa kinachompa nafasi ya kuendelea kufunga ndani ya kikosi chake cha Simba ni ushirikiano ambao anaupata kutoka kwa wachezaji wenzake.

Kagere ni kinara kwa kutupia ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa amefunga jumla ya mabao 13 na timu yake ikiwa imecheza mechi 23.

Kagere amesema: “Kikubwa ambacho ninakiona ni ushindani uliopo kwenye ligi kuwa bora kila siku, ninafunga kutokana na ushirikiano ambao ninaupata kutoka kwa wachezaji wenzagu.

“Tunacheza tukiwa ni timu, kila timu inapopata ushindi huo ni wetu sote bila kujali nani anayefunga, mashabiki nawapenda waendelee kutupa sapoti,” amesema.

Simba imefunga jumla ya mabao 47 kwenye ligi, Kagere amehusika kwenye mabao 18, akifunga 13 na kutoa pasi tano za mabao.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE