Home Uncategorized MZUNGU WA YANGA: TARATIBU WACHEZAJI WANAKUJA, WATAFANYA MAKUBWA

MZUNGU WA YANGA: TARATIBU WACHEZAJI WANAKUJA, WATAFANYA MAKUBWA

LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa atawajenga wachezaji wake kuwa katika hali ya kujiamini kwa muda atakaokuwa nao mazoezini na ana imani watamuelewa taratibu.

Kesho Yanga itakuwa na kazi ya kumenyana na Lipuli, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa ina kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar huku Lipuli ikiwa imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1 na Ruvu Shooting.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa ana amini katika uwezo wa wachezaji wake kutokana na kile ambacho wanamuonyesha uwanjani jambo ambalo linampa matumaini ya kupata matokeo kwenye mechi zake.

Kwenye jumla ya mechi nne ambazo amekaa benchi, Eymael ameshinda mechi mbili na kupoteza mechi mbili za Ligi Kuu Bara.

Alianza kwa kufungwa mbele ya Kagera Sugar mabao 3-0, akafungwa na Azam FC bao 1-0, alishinda mbele ya Singida United kwa mabao 3-1 na mbele ya Mtibwa Sugar kwa bao 1-0.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA YANGA AANIKA MIFUMO MITATU YA KIBABE