Home Uncategorized NYOTA MPYA WA MANCHESTER UNITED APEWA MUDA WA MWEZI MMOJA NA KOCHA...

NYOTA MPYA WA MANCHESTER UNITED APEWA MUDA WA MWEZI MMOJA NA KOCHA WAKE



QUIQUE Sanchez, aliyekuwa Kocha Mkuu wa nyota mpya wa Manchester United, Odion Ighalo amesema kuwa itamchukua muda wa mwezi mmoja mchezaji huyo kufikia mafanikio anayoyafikiria ndani ya Ligi Kuu England.
Sanchez alikuwa Kocha wa Odion wakati akikipiga ndani ya Klabu ya Watford na raia huyo wa Nigeria alitupia jumla ya mabao 17 ndani ya msimu alipokuwa akikipiga ndani ya Klabu ya Shanghai Shenua ya China kwa muda mfupi aliokuwa hapo.
Manchester United ina matumaini makubwa kwa nyota huyo mwenye miaka 30 ambaye ametua hapo kwa mkopo kuwa mbadala wa Marcus Rashford ambaye anasumbuliwa na majeruhi.
“Tatizo ni kwamba mafundisho aliyokuwa anayapata ndani ya ligi ya China pamoja na ligi ya England jambo ambalo linamfanya awe kwenye wakati mgumu kwenye mechi zake za mwanzo atahitaji muda wa mwezi mmoja kurejea kwenye ubora.
“Uzuri ni kwamba ninamtambua vema kwa upande wa uwezo wake ndani ya Uwanja pamoja na mwili wake ulivyo atafanya mambo makubwa,” amesema.

SOMA NA HII  KMC YAPANIA KUPEPEEUSHA BENDERA KIMATAIFA