Home Uncategorized SABABU ZA MAKOCHA MBAO FC KUBWAGA MANYANGA HII HAPA

SABABU ZA MAKOCHA MBAO FC KUBWAGA MANYANGA HII HAPA


HEMED Morocco na msaidizi wake Abdulmutik Hajji wameachana na timu ya Mbao FC ya mkoani Mwanza.

Morocco amesema kuwa sababu kubwa ya kuachana na tim hiyo ni matokeo mabovu ambayo wamekuwa wakiyapata.

Mbao FC ina pointi 19 ipo nafasi ya 18 imecheza mechi 22, imeshinda michezo minne, sare saba na imepoteza michezo 11.

Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njash amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kumtafuta kocha mpya atakayenoa kikosi hicho.


“Tunatoa shukran kwa kazi nzuri na ushirikiano waliotupa kipindi chote tulipokuwa nao na tunawatakia kila la kheri, kwa sasa tunafanya mchakato wa kumtafuta kocha mpya,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YAGOMA KUPEWA SABABU ZA KUSHINDWA, YAZIPIGIA POINTI TATU ZA KAGERA