Home Uncategorized SASA KICHUYA NDANI YA SIMBA MAMBO SAFI, HATMA YAKE MIKONONI MWA KOCHA

SASA KICHUYA NDANI YA SIMBA MAMBO SAFI, HATMA YAKE MIKONONI MWA KOCHA


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck ameshikilia hatma ya nyota wake Shiza Kichuya kucheza kwa sasa ndani ya kikosi hicho.
Kichuya ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Simba alikuwa anashugulikia suala la kibali cha kucheza soka ndani ya Bongo.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Uongozi wa Simba imeeleza kuwa hatma ya Kichuya kwa sasa kucheza ndani ipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Sven Vanderbroeck.
Kichuya alisajiliwa na mchezaji mwingine Luis Miquissone aliyekuwa akikipiga UD Songo yeye taarifa zinaeleza kuwa bado ITC yake haijatolewa na Simba wamepeleka suala hilo kwenye Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya FIFA.
Kichuya ambaye alikuwa mchezaji wa Simba na alijipatia umaarufu kwa kufunga bao la kona wakati Simba ikicheza na Yanga msimu wa 2016/17 na ngoma iliisha 1-1.
Alikuwa akikipiga ndani ya Klabu ya Ennpi ya Misri inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri, alirudishwa tena ndani ya Simba kwenye dirisha dogo la usajili wa msimu huu hakupata nafasi ya kutumika kwenye mechi nne za Ligi Kuu Bara ambazo zilichezwa hivi karibuni.
SOMA NA HII  AJIBU AWATAKA SIMBA WATULIZE BOLI, MSIMU NI WAO