Home Uncategorized TWIGA STARS KAZINI TENA KESHO, WAMETEMBEZA VICHAPO KWA WAWILI

TWIGA STARS KAZINI TENA KESHO, WAMETEMBEZA VICHAPO KWA WAWILI



MASHINDANO ya Kanda ya Kaskazini kwa Timu za Wanawake (UNAF) yanaendelea na kesho timu ya Taifa ya Twiga Stars itashuka uwanjani kumenyana na Morocco.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 9:15 alasiri nchini Tunisia na mchezo wa kwanza Twiga Stars ilishinda kwa mabao 7-0 dhidi ya Mauritania  na ule wa pili dhidi ya Algeria Twiga Stars ilishinda wa mabao 3-2.

Leo kikosi kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Academy ya Juventus kwa ajili ya kujiweka sawa na mchezo huo .

Bakari Shime, Kocha Mkuu wa Twiga Stars amesema kuwa morali ya wachezaji ipo sawa wanaamini watapata ushindi kwenye mchezo huo.

SOMA NA HII  ARGUERO AONGEZA URAFIKI NA NYAVU, KWA KUTUPIA TU BALAA