Home Uncategorized YANGA: HATUNA CHAGUO JINGINE ZAIDI YA KUTAFUTA USHINDI

YANGA: HATUNA CHAGUO JINGINE ZAIDI YA KUTAFUTA USHINDI


YANGA iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael, raia wa Ubelgiji, Februari 15 itakuwa na kibarua cha kumenyana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uatakaochezwa majira ya saa 1:00 Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa kwanza walipokutana msimu huu kwenye ligi, Yanga ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Patrick Sibomana Uwanja wa Samora, Iringa. Eymael amesema kuwa utakuwa ni mchezo mgumu ila watapambana kupata ushindi kwani hawana chaguo lingine.

“Kwetu sisi mechi zetu ni ngumu na ushindani ni mkubwa matumaini yetu ni kuona tunashinda ili kuongeza nguvu ya kufika kwenye malengo yetu tuliyojiwekea, hatuna chaguo lingine zaidi ya kutafuta ushindi” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na poiti 38 baada ya kucheza mechi 19.

SOMA NA HII  STERLING KUFIKIA KIWANGO CHA MESSI?