UONGOZI wa Mbao FC umesema kuwa kinachoikwamisha timu hiyo kuwa na matokeo mazuri ni ukata unaoimaliza timu hiyo yenye maskani yake Mwanza.
Mbao FC imecheza mechi 28 imeshinda mechi tano sare Saba na imepoteza mechi 16 ndani ya Ligi Kuu Bara .
Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi amesema kuwa suala kubwa la timu hiyo kuyumba ni kutokana na changamoto ya fedha.
“Tunajitahidi kuwa kwenye ubora wetu lakini tatizo ni fedha, gharama za uendeshaji ni kubwa nasi hatuna fedha za kutosha kwa sasa.
“Fedha za wadhamini kutoka kwa Vodacom na Azam TV tunashukuru tunazipata lakini bado hazitoshi. Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa sasa.
“Kuhusu udhamini wa GF Trucks hilo kwa sasa siwezi kuzungumzia kwani lipo nje ya uwezo wangu,” amesema.
Mbao FC ipo chini ya Kocha Mkuu, Ablumutik Haji, ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imejikusanyia pointi 22 kibindoni.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.