Home Uncategorized HIVI NDIVYO MSUVA WA EL JADIDA ALIVYOFANYA KUCHUKUA TAHADHARI YA CORONA

HIVI NDIVYO MSUVA WA EL JADIDA ALIVYOFANYA KUCHUKUA TAHADHARI YA CORONA

Habari za Michezo leo


SIMON Msuva, nyota wa Tanzania anayekipiga kwenye Klabu ya El Jadida ya Morroco amesema kuwa kutokana na kuchukua tahadhari ya kusambaa kwa Virusi vya Corona alipata muda mapema wa kuchukua vitu na kuweka ndani.

Kwa sasa dunia inapambana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinasambaa kwa kasi hata Tanzania pia ni miongoni mwa nchi zinazopambana na Corona ambapo Serikali ilitoa tamko la kuzuia mijumuiko yote isiyo ya lazima pamoja na kufunga shule na vyuo kwa muda wa mwezi mmoja.

Msuva amesema kuwa :” Serikali ilianza kutoa tahadhari mapema kuhusu Vrusi vya Corona nami pia nilifanya hivyo kwa kuchukua tahadhari mapema na kuchukua vitu sokoni na kuweka ndani.

“Kwa sasa sina wasiwasi kuhusu chakula na tahadhari pia ninachukua ili kuwa salama, kikubwa ni kuomba hali hii ipite ili turejee kwenye maisha yetu ya kawaida,”.

SOMA NA HII  KATWILA: DIRISHA DOGO TUTAFANYA USAJILI UTAKAOTUBEBA