Home Uncategorized SALAMBA AJIFUNGIA NDANI AKIPIGA MATIZI KULINDA KIPAJI CHAKE

SALAMBA AJIFUNGIA NDANI AKIPIGA MATIZI KULINDA KIPAJI CHAKE


ADAM Salamba nyota wa Tanzania anayeperusha bendera ya Taifa nchini Kuwait amesema kuwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona kwa sasa anapiga matizi ndani ili kulinda kipaji chake.

Salamba ambaye ni mshambuliaji amepewa dili la kuitumikia timu ya Al Jahra akitokea Klabu ya Simba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Salamba amesema kuwa kwa sasa hakuna ambaye anapata muda wa kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake kutokana na kusambaa kwa Corona.

“Hakuna ambaye anapata nafasi ya kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine zaidi mimi mwenyewe ninafanya mazoezi nyumbani tena ndani ili kuendelea kulinda kipaji changu,” amesema.

SOMA NA HII  KMC YATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA