Home Uncategorized DUH SASA BALAA KUTUA MSIMBAZI, NYOTA WANNE KIKOSI CHA KWANZA KUTIMKA MAZIMA

DUH SASA BALAA KUTUA MSIMBAZI, NYOTA WANNE KIKOSI CHA KWANZA KUTIMKA MAZIMA


IMEELEZWA kuwa baada ya kiungo bora ndani ya Simba,James Kotei kutimkia ndani ya kikosi cha Kaizer Chief kwa kandarasi ya miaka mitatu sasa nyota wengine watatu wanatimka ndani ya kikosi hicho.

Habari za ndani zimeeleza kuwa tayari kuna timu kutoka Afrika Kusini zimetia timu bongo kufanya makubaliano na wachezaji wa Simba.

Wachezaji hao wametajwa kuwa ni pamoja na beki Paul Bukaba na mshambuliaji Adam Salamba ambaye anahitajika kujiunga na Polokwane FC ya Afrika kusini.

Endapo madili yao yatakamilika yatafanya jumla ya wachezaji wanne kusepa ndani ya kikosi hicho kwa msimu huu.

Orodha yao itakuwa namna hii:-

James Kotei ametimkia Kaizer Chief.

Adam Salamba na Paul Bukaba wanawindwa na Kaizer Chief.

Haruna Niyonzima yeye amesema atatoa taarifa rasmi kwa timu atakayokuwa msimu ujao.

SOMA NA HII  NYOTA SABA WA YANGA WAIBUKIA UTURUKI