Home Uncategorized NDANDA YAKUTANA NA RUNGU LA TFF NAMNA HII

NDANDA YAKUTANA NA RUNGU LA TFF NAMNA HII


Timu ya Ndanda FC imetozwa faini ya Tsh 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi na kuliacha gari tupu likipita katika mlango rasmi katika mchezo uliofanyika Februari 29, 2020 uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.

Adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 14(43) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.


Mchezo huo Ndanda ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya wakata miwa ya Mtibwa.

SOMA NA HII  UNAAMBIWA HUYO YAO HAPO JANGWANI NI ZAIDI YA JESHI