Home Uncategorized SASA LIGI KUU BARA KUCHEZWA BILA MASHABIKI UWANJANI

SASA LIGI KUU BARA KUCHEZWA BILA MASHABIKI UWANJANI


KIKAO cha Kamati ya Uongozi cha TFF kimeazimia kuwa, baada ya siku 30 Serikali itakaporuhusu michezo kuendelea, mechi za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili na Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zitachezwa bila watazamaji, ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo mara baada ya kikao hicho ambacho kimehudhuriwa pia na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Kasongo amesema pia kuwa wachezaji wote watafanyiwa vipimo maalum kuchunguzwa endapo wameathirika na virusi vya Corona au la kabla ya ligi hizo kurejea.


Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, jana Machi 17 ilisitisha mwendelezo wa masuala yote ya michezo na mikusanyiko isiyo ya lazima ili kupambana na kasi ya kusambaa kwa Virusi vya Corona.

SOMA NA HII  MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMAMOSI, JUNI 22, 2019 HAYA HAPA