Home Uncategorized TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUSIMAMISHWA KWA LIGI KUU BARA, LIGI DARAJA LA...

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUSIMAMISHWA KWA LIGI KUU BARA, LIGI DARAJA LA KWANZA


KASSIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa wanasitisha masuala yote yanayohusu mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima ikiwa ni kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Majaliwa amesema:-“Tumesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile Ligi Kuu ya Tanzania, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la Kwanza, lakini pia michezo ya shule za msingi (Umitashumta), michezo ya shule za Sekondari (Umiseta) pamoja na ile ya mashirika ya umma. Michezo yote hiyo imesitishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo.

 “Kwa hiyo Wizara ya Habari na Utamaduni na Michezo yenyewe itawaandikia mashirikisho yake yote ya michezo ili kuwaambia kwamba kwa kipindi cha mwezi mmoja hiki watatakiwa kusimamisha ratiba hizo katika michezo inayochezwa kipindi hiki.”

SOMA NA HII  NAMUNGO WAMEDHAMIRIA KUSHUSHA MAJEMBE NANE YA KAZI, MMOJA KUTOKA YANGA