Home Uncategorized YANGA BABA LAO YAITUNGUA SIMBA YENYEWE YA KAGERE 1-0

YANGA BABA LAO YAITUNGUA SIMBA YENYEWE YA KAGERE 1-0

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga leo ametenda kazi yake iliyomleta Bongo kwa kuifunga Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Bao pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 44 kwa mpira wa adhabu alioupiga kiungo huyo raia wa Ghana na kuuzamisha mazima langoni baada ya Aishi Manula kuzidiwa nguvu na mpira huo.

Mpaka dakika 90 zinakamilka Simba ya Meddie Kagere ilishindwa kufurukuta mbele ya Yanga waliokuwa wakifanya mashambulizi ya hatari huku nyota wa mchezo kwa Yanga akiwa ni Metacha Mnata ambaye aliokoa michomo mingi ya hatari kwa Simba iliyokuwa ikipigwa na Meddie Kagere.

Ushindi wa leo unaifanya Yanga kufikisha pointi 50 ikiwa imecheza mechi 25 huku Simba ikiwa na pointi 68 imecheza mechi 27 za Ligi Kuu Bara

SOMA NA HII  AZAM FC YAWEKA PEMBENI HISTORIA YA YANGA, YAZITAKA POINTI TATU